Flicker Images

Happyness Watimanywa anaondoka nchini leo


Miss World Tanzania, Happyness Watimanywa anaondoka nchini leo hii kuelekea huko London Uingereza, tayari kabisa kwa maandalizi ya mashindano makubwa ya kumsaka mrembo wa dunia yatakayoanza rasmi tarehe 20, na kufikia kilele Desemba 14 mwaka huu.

 Katika muda atakaokuwa London, Happyness atajishughulisha pia na baadhi ya mambo ambayo yataitangaza zaidi Tanzania, na yeye binafsi ikiwepo mahojiano na baadhi ya vituo vya kimataifa vya habari. Happyness amesema kuwa, atamtembelea balozi wa Tanzania nchini humo kwa mualiko maalum, na pia atafanya mahojiano na vyombo vya kimataifa vya habari, ikiwepo BBC Idhaa ya Kiswahili.

0 Response to "Happyness Watimanywa anaondoka nchini leo "

Post a Comment