Flicker Images

Kuna tatizo kwenye ndoa ya Kim na Kanye? Kim arudi kwao kutoka honeymoon bila ya Kanye wala pete ya harusi

Baada ya kumaliza ndoa yao na harusi iliyofanyika wiki moja iliyopita, Kim na Kanye wanaonekana kuwa katika ugomvi baada ya kuonekana Kim akiwa peke yake alipotua uwanja wa ndege kuelekewa kwao LA.
Kim aliwasili New York siku ya jana (jumapili) bila ya mme wake Kanye alipokuwa akielea nyumbani kwao LA.
Inaonekana safari yao ya Honeymoon haikwenda vizuri kwa Kim na Kanye baada ya watoa habari kudai kuwa hawakuonekana wakifurahi na tabasamu zao zilikuwa kwa mbaaaali na wala hawakuwa wakioneshana upendo kati yao kwa muda wote waliokuwa honeymoon.

Habari zinadai kuwa Kim hakufurahishwa na idea ya Kanye kumpeleka Ireland ambapo kulikuwa na mvua nyingi kama sehem ya honeymoon yao.
Kim alioneka kuwa bored katika siku zote tano walizokuwa huko hata kumuomba Kanye waondoke mapema kabla ya siku hizo kuisha na hata kuachana na plan yao ya mwanzo ambapo walitegemea kupita Dublin kwa siku moja.
 Inaonekana kuna tatizo kwani Kim hakuoneka akiwa amevaa weeding band yake kidoleni


 "Nimeshawahi kupaona Ireland" aliskika akilalamika Kim "twende turudi".
Imeripotiwa kuwa Kim alipapenda Ireland mwaka 2012 wakati Kanye alipokwenda kwenye tour, na alienda kum-surprise Kanye  kwenye birthday yake alifikisha miaka 35.
Ndipo ambapo Kanye alipata idea yakumpeleka huko kwa kuwa alikuwa akiamini alipapenda na hata kupata sapoti kutoka kwa mama yake Kim ambae pia alienda huko wakati wa honeymoon yake ya Bruce Jenner mwaka 1991
 Kim akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa New York akiwa mwenyewe 


0 Response to "Kuna tatizo kwenye ndoa ya Kim na Kanye? Kim arudi kwao kutoka honeymoon bila ya Kanye wala pete ya harusi"

Post a Comment